Ufunuo wa Yohana 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 13 (Swahili) Revelation 13 (English)

Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Ufunuo wa Yohana 13:1

Then I stood on the sand of the sea. I saw a beast coming up out of the sea, having ten horns and seven heads. On his horns were ten crowns, and on his heads, blasphemous names.

Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Ufunuo wa Yohana 13:2

The beast which I saw was like a leopard, and his feet were like those of a bear, and his mouth like the mouth of a lion. The dragon gave him his power, his throne, and great authority.

Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Ufunuo wa Yohana 13:3

One of his heads looked like it had been wounded fatally. His fatal wound was healed, and the whole earth marveled at the beast.

Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Ufunuo wa Yohana 13:4

They worshiped the dragon, because he gave his authority to the beast, and they worshiped the beast, saying, "Who is like the beast? Who is able to make war with him?"

Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Ufunuo wa Yohana 13:5

A mouth speaking great things and blasphemy was given to him. Authority to make war for forty-two months was given to him.

Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Ufunuo wa Yohana 13:6

He opened his mouth for blasphemy against God, to blaspheme his name, and his dwelling, those who dwell in heaven.

Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Ufunuo wa Yohana 13:7

It was given to him to make war with the saints, and to overcome them. Authority over every tribe, people, language, and nation was given to him.

Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia. Ufunuo wa Yohana 13:8

All who dwell on the earth will worship him, everyone whose name has not been written from the foundation of the world in the book of life of the Lamb who has been killed.

Mtu akiwa na sikio na asikie. Ufunuo wa Yohana 13:9

If anyone has an ear, let him hear.

Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu. Ufunuo wa Yohana 13:10

If anyone has captivity, he will go. If anyone is with the sword, he must be killed.{TR reads "If anyone leads into captivity, into captivity he goes. If anyone will kill with the sword, he must be killed with a sword." instead of "If anyone has captivity, he goes away. If anyone is with the sword, he must be killed."} Here is the endurance and the faith of the saints.

Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Ufunuo wa Yohana 13:11

I saw another beast coming up out of the earth. He had two horns like a lamb, and he spoke like a dragon.

Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Ufunuo wa Yohana 13:12

He exercises all the authority of the first beast in his presence. He makes the earth and those who dwell in it to worship the first beast, whose fatal wound was healed.

Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. Ufunuo wa Yohana 13:13

He performs great signs, even making fire come down out of the sky to the earth in the sight of people.

Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Ufunuo wa Yohana 13:14

He deceives my own people who dwell on the earth because of the signs he was granted to do in front of the beast; saying to those who dwell on the earth, that they should make an image to the beast who had the sword wound and lived.

Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Ufunuo wa Yohana 13:15

It was given to him to give breath to it, to the image of the beast, that the image of the beast should both speak, and cause as many as wouldn't worship the image of the beast to be killed.

Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; Ufunuo wa Yohana 13:16

He causes all, the small and the great, the rich and the poor, and the free and the slave, to be given marks on their right hands, or on their foreheads;

tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Ufunuo wa Yohana 13:17

and that no one would be able to buy or to sell, unless he has that mark, the name of the beast or the number of his name.

Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita. Ufunuo wa Yohana 13:18

Here is wisdom. He who has understanding, let him calculate the number of the beast, for it is the number of a man. His number is six hundred sixty-six.